Kafyuu iliyopo kati ya saa mbili usiku na saa kumi alfajiri kwenye kaunti tano zinazoandikisha idadi kubwa ya maambukizi ya corona itasalia kuwepo hadi Mei 29.

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amesema kafyuu hiyo katika kaunti za Nairobi, Machakos, Kiambu, Kajiado na Nakuru ni sharti izingatiwe kikamilifu kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Amesema mikutano yoyote ya kisiasa au mikusanyiko ya aina yoyote inasalia kupigwa marufuku wakati huu.

Aidha kafyuu iliyoko katika kaunti zingine kuanzia saa nne usiku itasalia kuwepo na ni lazima izingatiwe.