Lawrence Warunge, mvulana aliyekiri kuwaua wazaziwe, nduguye, binamuye pamoja na mfanyikazi wa nyumbani mapema mwaka huu ako na akili timamu kushtakiwa kwa mauaji.

Ripoti ya uchunguzi wa kiakili iliyotolewa na hospitali ya Mathari imedhibitisha kwamba mshukiwa yuko sawa kiakili kushtakiwa kwa mauji hayo ya Januari mwaka huu.

Idara ya upelelezi DCI imesema Warunge,22, atashtakiwa katika mahakama kuu ya Kiambu Jumatano kwa mauji.

Mshukiwa wa pili, Sarah Muthoni ambaye ni mpenzi wake Warunge yuko huru kwa dhamana na atakuwa shahidi wa upande wa mashtaka.