Bunge linatazamiwa kumhoji waziri wa Fedha Ukur Yatani kuhusu kuongezeka kwa madeni yanayoendelea kuchukuliwa na serikali.

Kamati ya bunge kuhusu bajeti inatazamiwa kumuuliza waziri Yatani maswali ikiwemo mkopo wa hivi punde wa Sh263b kutoka kwa shirika la fedha duniani IMF.

Bunge linamuhoji waziri Yatani wakati ambapo baadhi ya Wakenya wameelezea kukasirishwa kwao na mikopo hiyo na kuiandikia IMF kusitisha mikopo hiyo kwa Kenya.

IMF inasema pesa hizo zinalenga kusaidia Kenya kupambana na janga la corona na kuinua uchumi uliotatizwa na janga hilo la kimataifa.