Carmen Hernandez,104, alipewa heshima kuu na wahudumu wa afya alipokuwa akiondoka hospitalini nchini Colombia. Kisa na maana? Amepona ugonjwa wa COVID-19 kwa mara ya pili.

Hernandez alipatwa na corona kwa mara ya kwanza Juni mwaka jana, na kisha akapatwa tena na ugonjwa huo Machi 8 baada ya kupewa chanjo.

Mara hii alilazwa hospitalini kwa siku 21 kabla ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Hernandez sio bibi wa kipekee kupona COVID-19.

Mnamo Januari, Hilda Brown, 102, alipona corona kabla ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na Anna Del Priore, 108 aliyeshinda corona mwaka jana.

‘’Najihisi vyema,’’Alisema Del Priore mwaka jana. ‘’Namshukuru Mungu niko mzima.’’