Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za kijamii yameishutumu serikali kutokana na kile yametaja kama kuminya uhuru wa kujieleza.

Yakijirejelea kukamatwa na kushtakiwa kwa mwanaharakati Edwin Kiama, mashirika hao ikiwemo KHRC yamezitahadharisha asasi muhimu za kikatiba kama vile mahakama dhidi ya kutumiwa na serikali kukandamiza haki msingi za kidemokrasia.

Wanjeru Nderu ni mmoja wa wanaharakati hao.

Kiama aliyekana mashtaka ya utumizi mbaya wa mtandao aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000 pesa taslimu.

Kiama anatuhumiwa kutengeneza bango lenye picha ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kulalamikia mikopo ya shirika la fedha ulimwenguni IMF.

Mabango hayo kisha yalisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii haswa na wakenya waliomuunga mkono.