Rais Uhuru Kenyatta amemuomboleza Mwanamfalme Philip aliyekuwa mume wa Malkia Elizabeth II aliyefariki akiwa na umri wa miaka 99.

Rais Kenyatta amemtaja mwanamfalme Philip kama mtu aliyekuwa nguzo muhimu katika umoja wa raia wa Uingereza na aliyekuza maadili mema ya kijamii.

Mwanamfalme Philip ambaye pia ni mtawala wa Edinburgh ametajwa kuwa mtu mwenye sifa za zamani, lakini pia alifahamika kwa mitindo iliyopitwa na wakati ya ucheshi usiofaa kisiasa, hali ambayo mara nyingine ilimfanya kuchekwa.

Prince Philip alimuoa Bintimfalme Elizabeth mnamo 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia, na alikuwa mwenza wa mfalme ama malkia aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia ya Uingereza.

Walikuwa na watoto wanne ,wajukuu wanane na vitukuu 10.