Uchunguzi umeanzishwa kufuatia kufariki kwa mtu mmoja baada ya kuripotiwa kupokea chanjo ya corona ya Astrazeneca.

Katika taarifa, bodi ya dawa nchini imearifu kuwa watu wengine saba wamepatwa na madhara na wako chini ya uangalizi wa madaktari.

Kwa ujumla, watu 279 wameripoti kupatwa na madhara mbalimbali ikiwemo kuumwa na kichwa.

Katika taarifa ya awali, wizara ya Afya ilisema madhara hayo hupotea baada ya siku mbili.

Jumla ya watu 325,592 wamepokea chanjo hiyo hadi kufikia sasa.

Miongoni mwao ni wahudumu wa afya wapatao 70,883, maafisa wa usalama 120,975, walimu 33,759 na watu wengine 115,903.