Mwanaharakati Edwin Kiama aliyekamatwa kwa madai ya kutengeneza bango lenye picha ya rais Uhuru Kenyatta kulalamikia mikopo ya shirika la IMF atajua hatma Alhamisi.

Mahakama imeamuru kuwa mwanaharakati huyo asalie rumande wakati mahakama itatoa uamuzi kuhusu iwapo au la ataachiliwa kwa dhamana.   

Kiama katika bango lake alidai kwamba fedha mbazo serikali hukopa hufujwa na maafisa wakubwa.

Wanaharakati wenzake wametumia mtandao wa twitter kuitaka polisi imuachie huru baada ya kushtumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa mtandaoni.