Magavana sasa wanalalama kuwa wamekosa pesa za kuwawezesha kuendelea kupambana vilivyo na janga la corona.

Kupitia taarifa iliyosomwa na gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyong’o, baraza la magavana linateta kuwa serikali kuu imechelewesha mgao wao wa Sh78b kuanzia Disemba mwaka jana na kufanya vigumu kwao kupambana na janga hilo.

Na sasa wanaitaka wizara ya fedha kuwatumia pesa hizo haraka upesi ikiwa ni kufikia Alhamisi wiki ijayo ili kuwawezesha kufanikisha vita dhidi ya janga hilo.

Baraza la magavana vile vile limeafikia kukutana na maafisa kutoka wizara ya afya Jumatatu wiki ijayo kujadili utata unaozingira uhaba wa dawa za kuzuia makali ya ugonjwa wa UKIMWI, ARVs.