Chama cha Mawakili nchini (LSK) kimewasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya serikali ya Kenya kupiga marufuku sekta ya kibinafsi kuagiza au kutoa chanjo ya corona.

Kwenye kesi yake, LSK inahoji kwamba uamuzi huo uliotangazwa na wizara ya afya unakiuka sheria kwa sababu serikali pekee haina uwezo wa kutoa chanjo kwa taifa nzima.

LSK kupitia kwa rais wake Nelson Havi inataka mahakama kutoa agizo linalozuia utekelezwaji wa uamuzi huo wa juma lililopita.

Chama hicho vile vile kinaitaka mahakama kubatilisha uamuzi wa kufutwa kwa leseni zilizokuwa zimetolewa kwa kampuni binafsi zilizokuwa zimeagiza na kutoa kutoa chanjo.