Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Dkt. Evans Kidero amesema amepatwa na ugonjwa wa corona wiki mbili baada ya kupewa chanjo dhidi ya virusi hivyo.
Kidero alipimwa pamoja na familia yake baada kuonesha dalili za ugonjwa huo.
Hata hivyo amesema familia yake wako salama ila yeye atajiweka kwenye karantini kwa muda wa majuma mawili kulingana na taratibu za wizara ya afya.