Baadhi ya wakenya wameisuta serikali kutokana na kuendelea kukopa madeni ambayo wanahisi yanawaongezea mzigo.
Kupitia kwa mitandao ya kijamii, wakenya hao wanalitaka shirika la Kimataifa la Fedha IMF kukoma kuipa serikali mikopo zaidi hadi pale serikali itakapowajibikia fedha ilizokopa.
Baadhi wanahisi kuwa kiasi kikubwa cha pesa hizo huishia mifukoni mwa maafisa wachache wa serikali badala ya kulifaidi taifa.
Hata hivyo naibu Mwenyekiti wa chama tawala cha Jubilee David Murathe ameitetea serikali kwa kuendelea kukopa haswa kutoka kwa IMF.
Katika taarifa, Murathe anasema mataifa mengi yanayoendelea yanategemea madeni na kuwataka wakenya kukoma kuingiza siasa kwenye suala hilo.
Haya yanajiri baada ya shirika la IMF kuidhinisha mkopo wa shilingi billion 255 kwa Kenya kusaidia kupambana na janga la covid19.