Maafisa wa polisi katika kaunti ya Busia wanamzuilia mshukiwa mmoja aliyenaswa akisafirisha vipatakalishi 71 vya wizi kuelekea nchini Uganda.

Evans Wanda, 24, alikamatwa mpakani na maafisa wa polisi kutoka Uganda akiwa anasafirisha mashine hizo kabla ya kupeanwa kwa maafisa wa Kenya.

Idara ya DCI inasema mashine hizo ziliibwa kutoka shule ya msingi ya Moding eneo la Teso, kabla ya usimamizi kupiga ripoti wiki iliyopita.

Mashine hizo zilikuwa na nembo ya serikali ya Kenya na inaaminika ni miongozi mwa zile serikali ya Jubilee iliwanunulia wanafunzi wa darasa la kwanza.