Muungano wa wanahabari nchini KUJ umelalamikia kudhulumiwa kwa mwanahabari mmoja katika kaunti ya Nakuru na maafisa wa polisi.
Mwanahabri huyo David Murunga anasema alikuwa anatoka kazini jana jioni baada ya saa mbili usiku wakati alidhulumiwa na maafisa wanne wa polisi ambao hawakuwa na sare rasmi.
Maafisa hao kisha walimkamata na kumpeleka kituoni licha ya kujitambulisha kuwa mwanahabari na hata kuwaonyesha vitambulisho vyake.
INSERT: MURUNGA ON ASSAULT
Kioko Kivandi kutoka muungano wa KUJ anasema inasikitisha kuona wanahabari wakidhulumiwa ilehali ni miongoni mwa maafisa ambao wana idhini ya kufanya kazi zao licha ya kuwepo kwa kafyu.