Kenya imeripoti maambukizi mapya 460 ya corona baada ya kupima sampuli 2,753 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Miongoni mwao ni mtoto wa miezi saba na hivyo kufikisha 139,448 idadi ya maambukizi nchini kufikia sasa.
Watu wengine 178 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 94,361 huku maafa ya wagonjwa 20 zaidi yakiripotiwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,244.
Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali nchini ni 1,590 huku wengine 5,998 wakishughulikiwa nyumbani.
Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi imeongzeka na kufikia 200, 40 kati yao wakisaidiwa na mashine kupumua.