Kwa mara ya kwanza tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini  Kenya imeshuhudia idadi kubwa ya maafa kutokana na corona.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amedhibitisha kuwa watu 28 wameaga katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,982

Watu 1,354 wamekutwa na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 7,732 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 118,889.

Idadi ya waliopona imefika 89,388 baada ya watu 185 kupona kutokana na ugonjwa huo.