Wizara afya imedhibitisha visa vipya 400 vya maambukizi ya corona baada ya kupima sampuli 5,189 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 107,729 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 87,176 baada ya kupona kwa watu wengine 77.

Waliofariki kutokana na ugonjwa huo wamefikia 1,873 baada ya wagonjwa watatu zaidi kufariki.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali nchini ni 494 huku wengine 1,615 wakishughulikiwa nyumbani.