Rais Uhuru Kenyatta ameitembelea familia ya aliyekuwa seneta wa Garissa Yusuf Hajji na kuifariji.
Marehemu Hajji alifariki Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mrefu na kisha kuzikwa katika makaburi ya Waislamu ya Langa’ta.
Katika rambirambi zake, Rais Uhuru Kenyatta amemtaja Haji kama kiongozi wa kutegemewa na mzalendo huku akitaja kifo chake kama pigo kwa taifa.
Kenyatta amesema Kenya itakosa uongozi wa Haji haswa katika mchakato wa BBI na kuiombea familia yake faraja.