Mahakama imesimamisha kwa muda mazishi ya mbunge wa Matungu Justus Murunga kufuatia kesi iliyowasilishwa na mwanamke mmoja anayedai kuwa mpenziwe marehemu.

Katika uamuzi wake, Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Agnes Makau anasema agizo hilo litasalia hadi pale kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mwanamke huyo Agnes Wangui ametakiwa na mahakama kuwapa maagizo ya kufika mahakamani wajane wa marehemu Christabel na Grace ili wahudhurie vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo Alhamisi wiki ijayo.

Wangui anadai kuwa mwendazake ni mumewe na wamezaa naye watoto wawili na kabla ya kifo chake alimtumia Sh1,300 kujaza gesi na Sh4,000 za matumizi.