Kwa mara nyingine waziri wa elimu Profesa George Magoha amewakanya walimu wakuu dhidi ya kuwafukuza wanafunzi shuleni haswaa watahiniwa kwa kukosa karo.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Busweta kaunti ya Vihiga, waziri  Magoha amesisitiza kuwa tayari wanafunzi wameharibu wakati mwingi wakiwa nyumbani kutokana na janga la corona na walimu wanafaa kuzingatia changamoto za kifedha zinazowakumba wazazi.

Waziri Magoha vile vile amesema wazazi wanafaa kupambana kulipa karo ya muhula wa pili kwani tayari muhula wa kwanza ulikuwa umekamilika wakati janga la corona lilibisha hodi nchini na kulazimu shule kufungwa.

Wanafunzi wanatarajiwa kurejea shuleni Januari mwaka ujao huku wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne wakiendelea na masomo yao.