Shughuli ya kukusanya sahihi milioni moja kwa ajili ya kufanyia katiba marekebisho kupitia BBI inatazamiwa kuanza wiki ijayo amesema kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Odinga ambaye anasema kuwa wanataka zoezi hilo liendeshwe kwa haraka ili waweze kukabidhi sahihi hizo kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC kabla ya safari ya kubadilisha katiba kukamilika kufikia mwezi Aprili mwaka ujao.

Akihutubia wanahabari Odinga pia amepuzilia mbali uwezekano wa maoni mapya kuongezwa kwenye ripoti hiyo siku moja baada ya maaskofu wa kanisa katoliki kutaka nafasi zaidi kutolewa ili ripoti hiyo ifanyiwe marekebisho.

Raila alikuwa akihutubia kikao hicho cha wanahabari baada ya kufanya kikao na viongozi kutoka Pwani ambapo pia wamezungumzia uchaguzi mdogo wa eneo bunge la msambweni huku akimkaribisha tena kwenye chama cha ODM Sharlet Mariam, ambaye alikuwa ametangaza kuwania uchaguzi huo kama mgombea huru.