Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuliongoza taifa katika maombi Jumamosi hii tarehe 10 kwenye hafla itakayoandaliwa katika Ikulu ya rais jijini Nairobi.

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena katika taarifa amesema viongozi wa madhehebu mbalimbali wanatazamiwa kuhudhuria maombi hayo ya kitaifa kuanzia saa nne asubuhi.

Wakenya pia wanahimizwa kutumia fursa hiyo ambayo ni Jumamosi na Jumapili kuliombea taifa linapoendelea kupambana na janga la COVID19.